Ronaldinho yupo tayari kuichezea Chapecoense


Klabu Chapecoense iliyo poteza wachezaji 19 waliofariki katika ajali ya ndege wakielekea Medellin kucheza fainali ya Copa Sudamericana, klabu hiyo inatarajia kumuona mchezaji maarufu duniani katika ngazi zake.

Akiwa huru , Ronaldinho ameonesha niya yake ya kujiunga na klabu hiyo baada tu ya habari mbaya iliyo tangazwa hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kama anavyo dai wakala wake '' Huu ni wakati mgumu sana katika klabu hii, tunajaribu kuisaidia Chapecoense. sijuwi kama itakuwa ni mechi ao mkataba, kama itakuwa ni mkataba tutajaribu kujadili.''

Naweza kusema kwamba  tupo hapa tunataka kuisadia klabu hii, kama jina la Ronaldinho limetajwa kwa mara ya kwanza, ni kwasababu anapendwa duniani pote na yupo huru pia anaweza kuwa mtu muhimu kwa kufuta majonzi ya mashabiki wa klabu hii. alisema wakala wa Ronaldinho.
Powered by Blogger.