Katika ulimwengu wa mitindo, mlimbwende kupata nafasi ya kushiriki
show ya Victoria’s Secret, ni sawa na muimbaji kupewa nafasi ya
kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy.

Herieth Paul (wa saba kutoka kushoto akiwa na warembo wengine wa VS
Kwa mara ya kwanza, mlimbwende wa Tanzania, Herieth Paul ameungana na
walimbwende wote maarufu duniani kwenye show hiyo kubwa, iliyopambwa
kwa aina yake na kufanyika jijini Paris, Ufaransa.

Herieth Paul akiwa kwenye chumba cha make up
Aliungana na warembo maarufu wakiwemo Kendall Jenner, Gigi na Bella
Hadid, Alessandra Ambrosio, Adriana Lima, Irina Shayk na wengine.