Wimbo mpya wa Diamond na Ne-Yo kupata airtime Marekani

Diamond Platnumz amedai wimbo wake mpya ambao haujatoka ‘Marry You’ aliomshirikisha Ne-Yo utachezwa mpaka kwenye vituo vya redio na runinga nchini Marekani.
13269419_1109188999169399_1336650774_n
Hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Salome’ amesema kuwa nyimbo nyingi za wasanii wa Afrika walizowashirikisha wasanii wa Marekani zimekuwa hazichezwi nchini humo.
“Namshukuru Mungu Ne-Yo kanitunuku ni kama bahati wimbo wangu uchezwe mpaka Marekani lakini kwa wasanii wengine wanakataaga,” amekiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.
Tayari video ya wimbo huo imeshafanyika tangu mwezi Septemba mwaka huu huko jijini Los Angeles, Marekani lakini bado haijajulikana muda wa kuachiwa rasmi.
Powered by Blogger.