WHITE PARTY: Msanii Dj Pro azungumzia sababu ya kiingilio ghali ya show yake


Msanii Dj pro kutoka Burundi mwenye makazi yake Afrika Kusini amefunguka kuhusu jambo inayo wasumbua wadau wake kuhusu kingilio ya show yake inayo subiriwa na watu wengi nchini Burundi. Decemba 17, 2016 ni tarehe inayo subiriwa na mashabiki wengi kwa kushuhudia bonge la show la msanii Dj Pro huku baadhi ya wadau wameanza kudai na kusema kuwa kiingilio ni ghali tofauti na show wanazo zowea nchi hapo.

Africanmishe imejaribu kutafuta dawa ya jambo hilo huku muhusika mwenyewe Dj Pro amefunguka nakusema kuwa Burundi inatubidi tubadilike ili tuwe sambamba na nchi zingine.

''Burundi tungali na kitu cha kujizarau sana na kwenye industry ya muziki icho sio poa kabisa, uwezi kuitwa star kila siku unafanya show ya elfu moja. Fanya kitu kikubwa ndio uitwe  star''.

Dj Pro amewahaidi mashabiki wa Burundi Flava kuwa atakaye kosa kwenye show hiyo basi hasitegemeyi kuona show kubwa tena nchini pia surprlise zitakuwepo nyingi sana.
Tuwakumbushe kuwa kwenye tiketi zote watapata chakula na vinywaji,  sehemu ya VIP kiingilio ni 50.000 za marundi huku pakiwa hofa ya chakula na vinywaji na upigaji wa Picha na ma star walio alikwa, sehemu ya kawaida kiingilio ni 25.000 za marundi pia hofu ni chakula na vinywaji, zaidi ya hayo itakuwa ni surprise kwa mjibu wa Dj Pro.

Powered by Blogger.