Walimu washinikiza kuhamishwa kukimbia ushirikina

Ukerewe. Hofu ya vitendo vya ushirikina imewafanya baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Uhuru wilayani Ukerewe, Mkoa wa Mwanza kushinikiza kuhamishwa.

Hali hiyo inatokana na mwalimu mwenzao, Charles Bwatwa kuanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa njiani kurejea nyumbani.

Kabla ya kifo cha mwalimu Bwatwa kilichotokea Oktoba 23, inadaiwa na walimu hao wamekuwa wakifanyiwa ushirikina na hasa usiku wakiwa wamelala.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Godwin Laurent amesema tangu kifo cha mwenzao, walimu wamekuwa wakiishi kwa hofu kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kagera, Alfaxad Kapole amelazimika kuitisha kikao cha pamoja kati ya walimu na wakazi wa eneo hilo kujadili madai ya kuwapo vitendo vya kishirikina.

Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Reginald Richard amesema kamati maalumu imeundwa kuchunguza ukweli wa jambo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha utoaji elimu kwa wanafunzi shuleni hapo.
Powered by Blogger.