Vyombo vya habari vya BBC, RFI vyapewa siku 30 DR Congo

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuna wasi wasi kufuatia sheria mpya nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambayo inavitaka vituo vya habari vya kigeni kujiandikisha kama makampuni ya nchi hiyo la sivyo matangazo yao yazimwe.

Waziri wa habari Lambert Mende amevipa vyombo vya habari siku 30 kutekeleza matakwa ya serikali
Waziri wa habari Lambert Mende amevipa vyombo vya habari siku 30 kutekeleza matakwa ya serikali
Sheria hizo mpya zitaanza kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.
Vyombo vya habari vya kigeni sasa vitaruhusiwa kutangaza nchini DRC, ikiwa asilimia kubwa ya wenye hisa ni raia wa Congo.
Maafisa wamevipa vyombo hivyo muda wa siku 30 kutekeleza matakwa hayo
Sheria hizo zinaathiri vituo kama Radio France Kimataifa (RFI) Sauti ya Amerika na BBC.
Matangazo ya RFI kwa sasa yamezimwa nchinin DRC, tangu itangaze mipango ya upinzani ya kufanya maandamano mapema mwezi ujao.
Powered by Blogger.