VIDEO:Cazorla ampa mbwa wake jina la mchezaji wa Manchester

Kupitia channel ya Youtube ya Arsenal, kuna video mbalimbali zinawekwa zikionyesha maisha
ya wachezaji wa Arsenal. Kwenye moja ya kipengele cha channel hiyo inamuonyesha mchezaji
Santi Cazorla akijibu maswali ya haraka ambayo wameita “Rapid Fire”
aliulizwa majina ya mbwa wake ambapo mmoja kati ya hao mbwa anamwita
Zlatan.
Kwenye moja ya maswali aliulizwa kwamba anamchagua Ronaldo wa sasa au De
Lima, Cazorla alijibu De Lima ni striker bora kutokea kwenye maisha ya
soka aliyoshuhudia. Kwa upande wa movie Cazorla alisema kwamba Loed of
Rings ndio movie bora kwake.
Kumpa jina la Zlatan mbwa wake kwake yeye ni moja ya njia za kuonyesha
jinsi gani anamkubali mchezaji huyo ambaye anacheza timu ya mahasimu wao
kwenye ligi ya England.
Hii hapa ni video kamili….
Powered by Blogger.