Video : Msanii Kebby Boy azidi kuitangaza Burundi nje ya nchi, ameanza namna hii kwenye Trace Mziki

 
Msanii Kebby Boy kutoka Burundi baada ya kufanya vizuri kwa kurikodi nyimbo kadhaa katika studio Wasafi Record ya Nyota wa bongo flava Diamond Platinum, ameanza arakati ya kubisha hodi nje ya nchi kwa kuitangaza bendera ya Burundi.

Kamwe watu hawataweza kukusifu ao kukubali kwa unachokifanya mpaka pale usipokuwepo kabisa, ni ajabu watu wengi hawajatambua kuwa wakionacho pekee ni kile wasichonacho, ni kile wanachokosa. Msanii Kebby Boy tayari amekwisha tambua ilo na ameanza kutafuta ajira za nje tofauti na wasani wengine.

Mkali wa My dodo, Keby Boy ameifungukia africanmishe kuwa amengundua zaidi ya muziki hakuna kitu kizuri kitakacho itangaza Burundi nje ya nchi, uku akisema kuwa kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa wasindikizaji tu.

Ni jambo tunahitaji warundi kuwa na msani wetu mkubwa mwenye hadhi na mafanikio kama Diamond Platinum na tukumbuke kuwa watanzania wenyewe ndio waliomfanya Diamond  kuwa msanii mkubwa kiasi hicho, basi Kebby Boy anaitaji warundi pia wafanye hivyo kwa wasani wao.

Ebu tazama hapa video, mahali ambapo Kebby Boy azidi kuongeza bidi yake pekee katika arakati ya kuitangaza muziki wa Burundi Flava nje ya nchi na tayari wameanza kuitambua kama Burundi kuna wasanii wenye vipaji vya hali ya juu.
Powered by Blogger.