Kiongozi
wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe katika kipindi cha Maswali
kwa Waziri Mkuu leo asubuhi  alidai kuwa, mnamo siku ya Jumanne tarehe
25/10/2016 saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM ambacho
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mwenyekiti, na kilihudhuriwa na
Katibu MKuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa ajili ya kujadili Muswada wa
Habari.

Mbowe
alisema kuwa Wabunge wakiwemo Mawaziri walihongwa shilingi milioni 10
kila mmoja ili waweze kusaidia kupitisha Muswada wa Habari unaotarajiwa
kuwasilishwa Bungeni kesho.

Lakini
Naibu spika alikataa  Waziri mkuu kujibu swali la Mbowe kwa  madai kuwa
swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa ni
rushwa kwa wabunge 
==> Wasikilize Hapo chini

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top