Valery Nahayo azungumzia sababu kubwa soka ya Burundi kufanya vibaya

 Katika maojiano na waandishi wa habari Jumamssi 29 Oktoba, Beki pia nahodha wazamani wa timu ya taifa Intamba Murugamba ( Burundi), Valery Nahayo alisema ukosefu wa fedha ni sababu kubwa inayo pelekea soka la Burundi kufanya vibaya.

Valery Nahayo alizaliwa April 15, 1984 mjini Bujumbura tarafani Buyenzi. Alianza kazi yake mwaka 2001 katika timu Atomic FC. Alijiunga na Muzinga FC mwaka 2002-2003  kabla ya kujiunga na Jomos Cosmos ya Afrika Kusini mwaka 2004.
 Aliisadia Jomos miaka kadhaa akiwa kama beki kitegemea  hadi 2008, mwishoni mwa mwaka 2008, aliondoka Jomos Cosmos na kujiunga na Kaizers Chiefs hapo hapo Afrika Kusini, hatimaye alisaini na Gent Belgium mwaka 2011. Miaka miwili baadae alirudi Afrika Kusini kwajili ya timu “Mpumalanga Black Aces”. 

Mke na watoto wake wanaishi kwa sasa Ubeljiji na familia yake. Valery Nahayo aliendelea kazi yake ya mpira huku akisoma ukocha (les cours d’entraîneur).

Alipoulizwa kuhusu hatma ya soka ya Burundi, Valery Nahayo amesema, 

Vijana wengi wanapenda mpira wa miguu, lakini wanakosa motisha. Mpira wa miguu nchini Burundi haulipi kadiri na mafunzo wanao ipata kwenye mazoezi, inabidi Serikali iwekeze fedha kwa kuhamasisha wachezaji.

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa Intamba Murugamba, alifunguka kuhusu swala la ukosefu wa makocha Burundi, nakusema
Ni kweli Burundi ina uwezo mdogo wakulipia kocha wa sifa kubwa, lakini sio tatizo kubwa hata kocha wa timu ya taifa anaweza kuipeleka Intamba kwenye hatua ya fainali, lakini vigumu inakuja ni kwamba hakuna  motisha itakayo mfanya kocha kufanya kazi yake vizuri.

Kuhusu namna gani inapashwa kuiandaa timu ya taifa, Valery Nahayo amesema

wachezaji wa Burundi wanakipaji cha hali ya juu ila wanakosa motisha fulani, ni changamoto kubwa kuona unaandaa timu ya taifa ya viana wenye umri chini ya miaka 17 baada ya miaka miwili baadhi ya vijana hauna nawo tena katika timu yako na miaka miwili baadaye wachezaji wote ni wapya. tatizo ni iloilo wachezaji wanashindwa kwakukosa motisha.


Aidha, mchezaji na kocha gani wa Burundi  anaye kubali mpaka sasa, Valery Nahayo amejibu,
wengi wanasema Maliki, ila sikumuona wakati anacheza, mchezaji ambaye nimeona kama ni bora ni
Constantin Kimanda, alikuwa bingwa wa Vitalo mwaka 1993-1998. Kocha bora ninaye kubali ni Kaze Cedric, aliongoza timu ya taifa na kwasasa anaendelea vizuri nchini Canada.

Tuwakumbushe kuwa kwasasa Valery Nahayo anaendelea kupata mafunzo ya ukocha katika shule ya makocha nchini Ubelgiji. Amehaidi akimaliza anapendelea kusaidia nchi yake, Burundi.


Powered by Blogger.