Universal Music Group walitoa dola milioni 1 (takriban shilingi bilioni 2.2 za Tanzania) ili kusambaza nyimbo za wasanii wa label ya Diamond Platnumz, WCBM, imefahamika.

Raymond na Diamond
Diamond ametoa habari hiyo kubwa leo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha XXL, Clouds FM. Meneja wake, Sallam ameiambia Bongo5 kuwa mkataba huo ulisainiwa tangu July mwaka huu lakini aliamua kutozungumza chochote hadi sasa.
UMG ambayo huingiza mapato ya zaidi ya dola bilioni 1 kila mwaka, ni label kubwa ambayo humiliki label zingine kubwa au hufanya kazi na label zingine (ikiwemo Def Jam Records). Label maarufu za wasanii ambazo kazi za wasanii wake husambazwa na UMG ni pamoja na Aftermath Records ya Dr Dre, Shady Records ya Eminem, Kon Live Distribution ya Akon, will.i.am Music Group, na zingine nyingine.
Kwa muda mrefu Diamond alikuwa na msimamo wa kutosainishwa na label yoyote labda kama mkataba ukiwa ni wa usambazaji pekee wa nyimbo za wasanii wa label yake, ambao UMG umempa. Roc Nation ni miongoni mwa label kubwa duniani zilizowahi kumtaka imsainishe lakini akazichomolea.
“Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond hivi karibuni kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.
“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”
“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine Diamond alidai kuwa kwenye album yake ijayo kuna nyimbo atakazowashirikisha Rick Ross na Rihanna.
Powered by Blogger.