Ukikutwa na mfuko wa plastiki Moshi, faini 50,000/-

WAKATI serikali ikiendelea kujipanga kudhibiti mifuko ya plastiki, Baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi limepitisha sheria

ndogo itakayodhibiti mifuko hiyo katika manispaa ya Moshi.

Awali wakati wa majadiliano ya namna bora ya kuipitisha sheria hiyo, baadhi ya madiwani waliipinga sheria hiyo,
wakiitaka manispaa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya mifuko hiyo.

Kufuatia mvutano huo uliodumu kwa zaidi ya dakika 30, Meya wa Manispaa hiyo, Raymond Mboya, aliamua madiwani hao kupiga
kura,  na kura 16 zilisema ndiyo, 10 hapana na mbili ziliharibika.

Mboya alisema, sheria hiyo  itawabana wafanyabiashara wa mifuko ambayo haina uwezo wa kuoza inapopigwa na jua na watakaokamatwa kutumia mifuko hiyo watalipa faini ya Sh. 50,000.

“Sheria hii ina mchakato mrefu ambao mbali na sisi kupitisha  kama madiwani bado zoezi hili linaweza kuchukua muda wa miezi sita hadi mwaka ili kusainiwa na Rais, jambo ambalo madiwani wote wanaweza kutumia muda huo kutoa elimu kwa wananchi  kuhusu mifuko hiyo,” alisema.

Colince Tamimu, Diwani wa Kata ya Soweto, alisema ni vyema sheria hiyo ikapitishwa ili kupunguza madhara yanayotokana na mifuko hiyo.

"Mifuko hiyo ya plastiki imekuwa kero kubwa kwa kuwa inaleta  madhara ya kiafya na uchafuzi wa mazingira,” alisema.

Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja,  walisema madiwani na serikali kwa ujumla wanapaswa kutoa elimu kwa jamii kuUkikutwa na mfuko wa plastiki Moshi, faini 50,000/-husu madhara ya mifuko hiyo.

“Ni biashara ninayoifanya kwa muda mrefu sasa ingawa nimesikia kuwa inapigwa marufuku, sina elimu ya kutosha juu ya
madhara hayo hali inayonipelekea kushindwa kuwaeleza wateja wangu…Nawashauri madiwani kupita katika kata zao na kuwaelimisha wananchi,” alisema Costanitine Masawe, mfanyabiashara wa mifuko ya
jumla.
Powered by Blogger.