Tunda asema Nimefanya video karibia 10 lakini ya Diamond mnaniuliza kila saa, who is Diamond motherf****Tunda amechoka kuulizwa maswali kuhusiana na kuonekana kwenye video ya Diamond ya wimbo Salome aliomshirikisha Ray Vanny.

Ni kwasababu anajiuliza, iweje ameshaonekana kwenye video takriban 10, lakini tangu aonekane kwenye video ya Diamond, swali limekuwa lile lile na ni kama vile watu ndio wameanza kumuonea kupitia video hiyo.
14716636_1787141504900898_235544725296250880_n
Kutokana na kuchoshwa na swali hilo, Tunda anayedaiwa kurudiana na mpenzi wake Young Dee, amempa jibu kavu mtangazaji wa Jembe FM, Natty E aliyemrushia swali lile lile limkeralo.
“Nimefanya video ngapi? Nimefanya video karibia 10 lakini hii ya Diamond mnanifanyia interview kila saa,” Tunda alimjibu Natty.
“Diamond, Diamond, who is Diamond motherf*cker. Weka hiyo kwenye gazeti lako,” aliongeza.
15258734_1627592057542024_4426690412505202688_n
Natty alijikaza na kumjibu ‘Anyway, Unaweza acha hilo swali la kuhusu Diamond, it’s not a big deal.’
Tunda alijibu kikauzu zaidi, “Maswali yote jibu lake ndio hilo.”
Powered by Blogger.