TB Joshua ni mmoja wa wahubiri mashuhuri zaidi barani Afrika

Utabiri kutoka kwa mhubiri raia wa Nigeria TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani, umerejeshwa tena baada ujumbe huo kufutwa kutoka mtandao wa Facebook.

Kulingana na barua pepe iliyotumwa kwa BBC na idara ya mitandao ya kanisa la TBJMinistries ilisema kuwa , "ujumbe huo uliondolewa kimakosa na sasa umereswa kwa kuwa hiyo si sera yetu."

"Siku kumi zilizopita nilimuona rais wa Marekania akishinda kwa kura chache, yule niliyemuona ni mwanamke," ujumbe huo ulisema.

TB Joshua alikejeliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakati watu walitambua kuwa ujumbe huo ulikuwa umefutwa, licha ya wafuasi wake wengi katika mitandao ya kijamii bado kumtaja kuwa nabii.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top