Tamthilia ya JB ‘Kiu ya Kisasi’ kuingia mtaani, Naj wa Barakah The Prince ndani

Mtayarishiji wa filamu na mwigizaji, Jacob Stephan ‘JB’ amewataka mshabiki wa filamu kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa tamthilia yake mpya ‘Kiu ya Kisasi’ ambayo ipo katika hatua ya mwisho ili kuingia sokoni.
14915279_1231589280235715_1128545704624706176_n
Tamthilia hiyo imewakutanisha mastaa mbalimbali akiwemo, Naj na pamoja na wengine.
Kupitia instagram, JB ameandika

Niko katika hatua za mwisho kabisa za editing ya tamthilia yetu ya kiu ya kisas ni90%imekamilika..tutatangaza wapi tuta rusha kazi hii..sina kawaida ya kusema uongo..kazi hii ni nzuri sana…inatosha kuwafanya mtoroke kazini..itaruka kwa mwaka mzima kwani tuna zaidi ya episode 50 za kusisimua…pichani ni baadhi ya washiriki…#kiuyakisasi …inakuja toka jerusalemfilms.
Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri sokoni na filamu ya Kalambati Lobo, ataachia filamu yake ya mwisho na baada ya hapo ataachana na kuigiza nakubaki kama producer.
Powered by Blogger.