Rapper wa kike kutoka nchini Kenya,Femi One aeleza kwanini muziki wa Kenya haufanyi vizuri kimataifa

Rapper wa kike kutoka nchini Kenya, Femi One amefunguka na kueleza sababu ya muziki wa nchi hiyo kushindwa kufanya vizuri kimataifa tofauti na miaka ya nyuma.
14736394_193523564429838_6064226361453576192_n
Femi amedai kufanya vizuri kwa muziki wa Nigeria kwa sasa kwenye nchi za Afrika ndio kumesababisha muziki wa nchi yao kushuka.
Akiongea na Bongo5, rapper huyo amesema, “Kwa sababu muziki wa Nigeria umekuja na kutake over, wanapewa airplay sana huku kuliko muziki wa Kenya. Na msanii wa nje akija hapa Kenya anapokelewa vizuri na kulipwa fedha nyingi kuliko msanii wa hapa.”
Rapper huyo ambaye anafananishwa na Nazizi, ameachia video yake mpya ya wimbo ‘Jah’ akiwa chini ya Kaka Empire.
Powered by Blogger.