Muhimbili kuanza upasuaji watoto wasiosikia na kuongea

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), itaanza kufanya upasuaji kwa watoto wasuozungumza na wasiosikia kwa ajili ya  kuwawekea kifaa maalum cha kuweza kusikia na kuongea.

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amesema huduma hiyo itaanza kutolewa Januari  mwakani.

Amesema wagonjwa hao wamekuwa wakitibiwa nje ya nchi. Amesema baada ya kuanza kutolewa kwa huduma hiyo watoto waliozaliwa wakiwa hawasikii wa kuongea wataweza kufanya hivyo.

Amesema gharama kwa huduma hiyo nchini India inafikia Sh100 milioni wakati hapa nchini itakuwa pungufu kwa kati ya asilimia 40 hadi 50.
Powered by Blogger.