Muasisi wa Nyama Choma Festival azungumzia kuigwa kwa tamasha hilo Kenya na jinsi lilivyokuwa kubwa

Katika maisha kila kitu kizuri huigwa. Haijawa tofauti kwa tamasha la Nyama Choma ambalo limegeuka kuwa shughuli kubwa nchini katika kipindi cha miaka michache tu.
a23b5345-5f42-45f4-bee6-b0097ed07b63
Hivi karibuni, walijitokeza waandaji wengine wa Kenya waliokuja na wazo kama hilo na kuliita hivyo hivyo. Kama haitoshi, watu hao waliiga hadi aina ya graphics zinazotumika katika tamasha la Tanzania.

Nimezungumza na Carol kutaka kujua wanachukuliaje kuigwa na pia lilipofika tamasha hilo.
Umejisikiaje kuona wazo lako la Nyama Choma likiigwa vile vile kama ambavyo wewe unafanya?
Wanasema ‘imitation is the highest form of flattery’ yaani ukiona unaigwa ujue unachokifanya ni kizuri au kina manufaa. Hata hivyo inasikitisha sana kuwa wanaoiga hawataki hata kujiongeza kwa lolote, wanachukua wazo kama lilivyo na kubadilisha tu jina kidogo. Hamna wazo jipya chini ya jua, lakini kunatakiwa kuwa na utofauti utakaokutambulisha wewe na chapa yako. Tuheshimu kazi za watu pia ndio la msingi kuliko yote.

Hii neno ‘Nyama Choma Festival’ ni brand ambayo uliibuni mwenyewe ama iliwekupo awali sehemu nyingine?
‘The Nyama Choma Festival’ ni jina tulilokuja nalo wenyewe, na kwa kipindi hicho kulikuwa na ‘Nyama Choma Competition’ ambayo haki miliki na wazo halisi iko chini ya TBL. Kuna ‘Barbecue Festival’ Marekani na Australia, lakini kwa Tanzania ‘Nyama Choma Festival au Barbecue Festival’ ni chapa yetu sisi. Pia ndio maana tukaiita ‘The Nyama Choma Festival’ ili watu waweze kutofautisha,msisitizo ukiwa kwenye ‘The’,kusisitiza kuwa hii ndio original.
14597496_200843853676290_4707304553215688704_n
Carol Ndosi


Kuna hasara gani kwa Kenya kuchukua wazo kama hili? Ulikuwa na mpango wa kuipeleka huko wewe mwenyewe?
Bahati mbaya Kenya walituiga miezi 3 tu baada ya kuanzisha ya kwetu 2011. Uzuri wao huko huko wana malumbano maana tayari kuna matamasha 4 yanafanya kitu hicho hicho. Tumesajili ‘The Nyama Choma Festival’, na tukihakikishiwa udhamini utatusikia na sisi tumewafikia. Tunajivunia chapa yetu inajulikana Afrika Mashariki nzima na hivyo jina letu TNCF linajiuza lenyewe.
Kuna hatua yoyote unafikiria kuchukua kwa kunakiliwa kwa wazo la biashara yako nje ya nchi?
Hatua ni kusajili kwanza na kupata haki miliki ya jina na wazo halisi. Tunaendelea na mchakato Rwanda,Uganda na Congo. Inachukua muda sababu tunatafuta loyal local partners pia.
Tamasha la Nyama Choma limekuwa kubwa kwa kiasi gani na ulitegemea ungefika hapo leo?
2017 tunatimiza miaka 6. Tunatoa ajira kwa watu zaidi ya 2000 kwa siku Dar es Salaam. Wahudhuriaji wameongezeka toka 700 tamasha la kwanza hadi 20,000 kufikia mwaka 2015. Tunashukuru Mungu jitihada zetu zinaendelea kufanikiwa katika kuhakikisha tunaijenga TNCF kama chapa ya kujivunia Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Powered by Blogger.