Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Allan Mapigo amesema kuwa wasanii wengi wanavurunda kwenye show zao kutokana na kukosa nidhamu.

18341292_303
Akizungumza katika kipindi cha Ladha 3600 cha EFM wiki hii, Mapigo amedai wasanii wengi wanajali kupendeza stejini kuliko kuboresha show zao.
“Hata mimi nilikuwa na mpango wa kutoa darasa la production kupitia ukurasa wangu wa instagram, Wasanii wengi wanavurunda kwenye show kwa kukosa nidhamu ya muziki wanachopenda ni bring bring tu na kupost kwenye mitandao,” alisema Mapigo.
“Katika kizazi hiki wapo pia watayarishaji wazuri wanafanya kazi bora pengine hata kuzidi zile tulizowahi kufanya hapo nyuma, Lakini pia wapo wasanii wanao”copy” sana kiasi cha kushindwa kuwatofautisha”
Allan ni mmoja kati ya watayarishaji wakongwe wa muziki ambao wameandaa nyimbo nyingi za wasanii wa dansi na bongofleva.
Powered by Blogger.