Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema kiama cha blayback kimefika hivyo wasanii wajifunze kupiga muziki wa live kwenye show zao.

Rapa huyo ambaye alifanya show ya live katika tamasha la Fiesta lililofanyika weekend iliyopita, amesema amegundua kuna kitu cha ziada wanapata mashabiki wake kutokana kuimba live kwenye show.
“Kusema kweli nimepata pongezi kutoka kwa watu wengi sana tena wengine sina ushikaji nao,” alisema Dogo Janja. “Kwahiyo kwangu mimi naona kwa sasa ndo muziki unaenda huko, kiama cha playback kimefika, wasanii tubadilike twende kwenye muziki ambao unaweza kupendwa na dunia,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa kazi zake mpya.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top