TANGAZO
Hakeem 5
Msanii wa bongo fleva Hakeem 5 amesema hawezi kumuomba Ali Kiba msamaha kwa kuwa hajafanya kosa lolote na alichoongea kuwa Ali Kiba anaroho mbaya aliongea ukweli.
Akiongea ndani ya eNewz amesema anaweza kuishi akiwa anafanya muziki na hata  asipofanya hivyo anaweza akaishi hivyo hawezi kwenda kumuomba Kiba msamaha kwa kuwa yeye hakutaka kufanya kolabo na Kiba ila Kiba ndiye alimuomba wafanye kolabo.

Hata hivyo Hakeem 5 hakusita kumjibu Abby Skills na kumuambia kuwa aache unafiki na aendelee na mambo yake kwani hajui chanzo na angekuwa anataka amani angekaa akawapatanisha kama ndugu na siyo kukaa na kuanza kumkandamiza kwenye vyombo vya habari.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top