Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief kufanya kolabo na Patoranking wa Nigeria

Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa wimbo wake mpya aliomshirikisha Patoranking wa Nigeria.
Q Chief
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Q Chief amedai wiki ijayo atasafiri kuelekea Nigeria kwa ajili ya kukamilisha project hiyo.
“Tayari ndani kuna kazi nyingi ambazo zinakuja ukiachana na ile ambayo nimefanya Afrika Kusini kuna kolabo inakuja nikiwa na Patoranking,” alisema Q Chief. Mungu akipenda wiki ijayo nitasafiri pamoja na uongozi wangu kwenda Nigeria kwa ajili ya kukamilisha project hiyo,”
Aliongeza, “Kwa sasa nimeshindwa kuachia project yangu niliyofanya Afrika Kusini kutokana na haya matamasha ambayo yanaendelea, lakini naweza kusema hakuna kitu ambacho kimeharikika kwa sababu hali ikikaa sawa tunaanza kuachia ngoma tena naweza nikaanza na kolabo yangu na Patoranking,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mkungu wa Ndizi’ amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kutoka kwake.
Powered by Blogger.