Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi afuta vyama vitatu vya siasa

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi 
Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi  amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutowasilisha ripoti za ukaguzi wa hesabu za fedha.

Sababu nyingine ni kutokuwa na ofisi na kushindwa kuthibitisha kuwa na wanachama Zanzibar

Amevitaja vyama hivyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta) kilichokuwa kinaongozwa na James Mapalala na The Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) kilichokuwa kinaongozwa na Peter Mziray kama Rais Mtendaji.

Chama kingine kilichofutiwa usajili ni Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari kama Mwenyekiti taifa

Source: Mwananchi
Powered by Blogger.