TANGAZONa .Vero Ignatus ,Arusha.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay amepokea msaada wa mashine mbili za kusomea kwa wanafunzi wenye uoni hafifu (Magnifier Machine) zenye thamani zaidi ya Tsh Mil 10 toka kwa wanachama wa Lions Club “Arusha City branch”.

 Akipokea Msaada huo toka kwa Gavana Vinie Tinkumanya toka Uganda ambaye ni mwananchama wa Club aliyeongozana na wanachama wa Arusha City Lions Club alielezea furaha yake kupokea mashine hizo na kuwashru Club hiyo kwa kufikiria na kukumbuka kundi maalumu la wanafunzi wenye uoni hafifu (Low vision)

 “Tumekuwa tukipokea misaada mingi lakini ni mara chache sana wafadhili kuwambuka vijana wetu hawa, mmetoa msaada wenye thamani sana kwa Jiji la Arusha na mmeonyesha upendo wa hali ya juu kwa watoto wetu”alisema Meya Bukhay. 

 Aliongeza kuwa pamoja na shukrani hizi pia naomba ikiwezekana mtupatie na misaada zaidi ya ajili ya Elimu maalumu kwa kuwa tuna mahitaji makubwa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya watoto wetu wa Elimu maalumu. 

 Naye Gavana Tinkumanya alisema kutoa misaada ndio nguzo ya Club yao na wanapenda kuwafikia watu wengi zaidi kwa kugusa maisha yao na kuwawezesha kupitia misaada mbalimbali ya kijamii, Kielimu hata kiuchumi. 

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top