Messi na wenzake wagomea wanahabari Argentina

Lionel Messi amewaongoza wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kususia kuongea na wanahabari baada ya uokosoaji kuhusu uchezaji duni wa timu hiyo.Lionel Messi
Messi, 29, alitangaza mgomo huo baada yake kufunga bao wakati wa ushindi wao wa 3-0 mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Colombia.
Kituo kimoja cha redio kilikuwa kimeripoti kuwa mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi baada ya kipindi cha mazoezi, tuhuma ambazo amekanusha.
"Tumepokwa tuhuma nyingi, kukosewa heshina na hatujasema lolote," messi alisema.
Messi na wenzake 25 waliondoka kutoka kwenye kikao na wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi hiyo dhidi ya Colombia.
Taarifa zinasema Lavezzi atakishtaki kituo hicho cha redio.
"Tunajua wengi wenu ambao hamna heshima kwa mchezo huu, lakini kuingilia maisha ya kibinafsi ya mtu mmezidi," Messi aliongeza.
Argentina walikosolea sana baada yao kulazwa 3-0 na Brazil lakini ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Mataifa manne yanaomaliza juu kanda ya Amerika Kusini hufuzu moja kwa moja. Nambari tano hukutana na mpinzani kutoka bara jingine kuamua mshindi.
Powered by Blogger.