MC Koba na Mwana FA walaani nyimbo za Nigeria kutawala shindano la Miss Tanzania

Mapya yanazidi kuibuka kwa kulitoa kasoro shindano la Miss Tanzania 2016 lililofanyika Jumamosi iliyopita jijini Mwanza. Wadau wa muziki wamekasirishwa kwa kitendo cha kuchezwa nyimbo nyingi za wasanii wa nje.
0-1jembe-balaa13
Msanii wa Bongo Fleva aliyekuwa kwenye kundi la Watu Pori la Morogoro, MC Koba amesema kuwa ni aibu kwa tukio kubwa kama hilo la kitaifa kuchezwa kwa nyimbo nyingi za wasanii wa nje.
“Mimi binafsi imeniuma sana kama msanii na nimeonewa sasa, tena inawezekana siyo peke yangu. Lile ni tukio la kitaifa. Kitendo kwa tukio kubwa kama hili la kitaifa kupigwa kwa nyimbo nyingi za nje. Sisi tutathaminika vipi wakati hatuvithamini vyakwetu?,” amekiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.
Kwenye ujumbe mwingine Koba anasema:
Muziki wetu unakwenda wapi, kwa mwendo huu nani wa kumlaumu huko mbele kama tusipochukua maamuzi muhimu sasa? Suala la kutumika kwa beat na nyimbo nyingi za kinaijeria kwenye shindano la kutafuta mrembo wa Tanzania mwaka 2016 lililokuwa likiruka live kwenye TV zaidi ya moja ni kuikosea heshima tasnia ya muziki wetu. Yeyote aliyehusika kwenye kuchagua nyimbo za kutumika jukwaani wakati mamiss wanashindana ametukosea wa Tanzania kwa mtazamo wangu.
TV zetu zinafika nchi jirani na kwingineko kama walifuatilia wanatuchukuliaje? Watathamini vipi chetu tunachopambana kuwapeleka kama sisi tunathamini cha nje? Nilitegemea serikali iseme lolote juu ya hilo mwakilishi wa wizara alikuwepo akapiga kimya halafu wanatubana kwenye kodi huku hawatutengenezei mazingira ya kulinda muziki wetu what sense does it make? Zipo hit songs kadhaa pengine zingeweza kutumika Salome Diamond, Aje Ali kiba, Moyo Mashine, Ben Pol na kadhalika kulikuwa na sababu gani ya msingi kutumia mdundo wa tecno pale stage?
Kwa upande wake Mwana FA ameandika kwenye Twitter: Muziki wao kwenye redio zetu, TV zetu, madisco yetu, sasa mpaka kwenye mashindano ya mrembo wa nchi yetu.”
Powered by Blogger.