Maguli ameeleza tofauti ya soka la Tanzania na Oman

Aliyekua mshambuliaji wa klabu za Ruvu Shooting, Simba SC pamoja na Stand United Elias Maguli ameelezea tofauti ya uendeshaji wa soka wa Tanzania na Oman anakocheza soka kwa sasa katika klabu ya Dhofar FC.
img_0677
Maguli ambaye aliondoka nchini mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia Mashariki ya Kati amesema kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa soka ambao amekutana nao nchini Oman.
Amesema mfumo wa maisha ya soka nchini humo unatoa nafasi kubwa kwa wachezaji kuwa na uhuru wa maisha yao, jambo ambalo kwa hapa nchini limekua tofauti kutokana na timu kuwa kambini karibu msimu mzima wa ligi.
“Tanzania tumezoea kukaa kambini kuanzia mwanzoni mwa maandalizi ya ligi mpaka mwishoni mwa ligi, kwa wenzetu ni tofauti kidogo, tunafanya mazoezi na kurudi nyumbani,” anasema mshambuliaji huyo aliyewahi kutemwa Simba kwa mizengwe.
“Tunaingia kambini siku moja kabla ya mechi wakiamini kwamba mpira ndio kazi yako kwahiyo na mpira ni mchezo wa hadharani performance yako uwanjani itaonesha kilakitu.”
“Lakini nyumbani ni tofauti kidogo, wachezaji lazima wakae kambini kwasababu viongozi wanadhani wakiwaachia watafanya mambo mengine nje ya uwanja.”
Maguli aliwahi kufanya vizuri akiwa na klabu ya Ruvu Shooting na kuwashawishi viongozi wa Simba kumsajili lakini wakamtema baada ya muda mfupi bila sababu za kimpira. mshambuliaji huyu mwenye misuli iliyojengeka kimazoezi akajiunga na Stand United na kuendeleza moto wa kucheka na nyavu kabla ya kuelekea Oman kucheza soka la kulipwa.
Powered by Blogger.