Maelfu waandamana kumtaka waziri mkuu wa Malaysia ajiuzulu

Najib Razak alaumiwa kwa kuhusika kwenye kashfa ya ufisadi

Maelfu ya watu nchini Malaysia wamemiminika katika bara bara za mji mkuu wa Kuala Lumpur, kumtaka waziri mkuu Najib Razak, kujiuzulu kutokana na madai ya kuhusika kwake na na kashfa ya ufisadi.

Bwana Razak amekanusha madai hayo lakini makundi ya kutetea haki yanasema amekuwa akiwahujumu wakosowaji wake.

Wanaharakati wa kupigania demockasia wameandamana kati kati ya mji huo wakiimba na kupiga ngoma.

Zaidi ya maafisa wa polisi elfu saba wamepelekwa karibu na maeneo kunakofanyika maandamano hayo.
Powered by Blogger.