Kocha wa timu ya Mkoani Gitega Musongati, Vivier Bahati aridhika kwa kupata suluhu (0-0) dhidi ya timu ya taifa.

Kocha Vivier Bahati
Jumamossi Novemba, 19, 2016, mkoani Gitega, Timu ya taifa Intamba Murugamba imejielekeza mkaoni hapo kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Musongati ya kocha Vivier Bahati,  upande wote mbili ilitafuta angalau goli moja bila mafanikio.

Kocha wa Musongati ameridhika na matokeo ya suluhu (0-0) huku akisema kuwa timu yake imekua likizo ya wiki moja ila timu ya taifa hipo kambini wiki mbili, matokeo upande wake ni sawa.

naridhika na matokeo ya leo dhidi ya timu ya taifa na unajua kuwa timu yangu imekuwa likizo wiki moja  ila timu ya taifa hipo kambini wiki mbili sasa. tulianza mazoezi wiki hii na leo tumecheza mechi vizuri kwa kweeli nafurahi na kiwango cha wachezaji wangu, amesema Kocha Vivier Bahati
Kuna baadhi ya wachezaji wa Musongati wameitwa mu timu ya taifa kwa kuanda michuano ya cecafa na Chan ila kwenye mechi ya kirafiki wachezaji hawo wamechezea klabu yawo huku kocha Vivier amezidi kuwapongeza wachezaji hawo nakusema kuwa wameleta mutisha mkubwa na kuwasaidia wenzao kuwa sawa kwenye mechi hiyo.

ndio wachezaji wangu walio itwa na timu ya taifa wameisaidia sana Musongati katika mechi ya leo, ninaimani wataleta mchango mkubwa kwenye timu ya taifa endapo watasalia kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Kocha Vivier Bahati ameifungukia Africanmishe kuhusu kuwa na mashabiki wengi mkoani hapo mwaka huu tofauti na miaka za nyuma,

ndio mashabiki wanajitokeza kwasana kwa sababu ya matokeo yetu mazuri, na tunawaimiza waje wengi kwa kuisapoti timu yawo na pia kila mechi kuna mchango fulani unapitishwa kwa kila shabiki ili mwisho wa mwezi tuwape wachezaji mshahara wao bila kuchelewa na ndio sababu kila mchezaji anajituma uwanjani.

Aidha, nini aswa siri ya mafanikio ya Musongati kuonesha kiwango kizuri kwenye ligi kuu msimu huu? kocha vivier amejibu nakusema

kwanza mashabiki ni wengi wanaipenda timu yawo, najitaidi kutumika kwa hali na mali kadiri ya uwezo wangu kama kocha ili nifanikishe malengo ya timu na ninaimani siku za mbele Musongati itaonesha mpira mzuri tofauti na munavyo shuhudia leo.

Tuwakumbushe kuwa Kocha Vivier Bahati ndiye naibu kocha wa timu ya taifa na anaendelea kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa soka kama kocha.

Powered by Blogger.