Kocha wa Musongati Vivier Bahati azungumzia kuhusu mechi ya Vitalo na wiki ijayo dhidi ya Atletico Olympic

Kocha Vivier Bahati                                       
Ligi ya Burundi imeingia katika wiki yake ya 11 huku mechi ya kusisimua imekuwa ni kati ya wabingwa watetezi Vitalo dhidi ya Musongati kutoka mkoani Gitega; timu zote mbili zimetoka suluhu (0-0).

Baada ya kuitambia Inter Star  bao tano bila wiki mbili zilizo pita, timu ya Musongati inakua timu tishio na  jana imechuana na Vitalo katika mechi nzuri ya kupendeza pande zote mbili.
Timu zote zimejaribu kuona lango bila mafanikio pia Musongati imemaliza mechi ikiwa inapungukiwa na mchezaji wake mahiri Sudi ambaye amepewa kadi nyekundu kipindi cha pili hata ivo Musongati imesalia imara zaidi na kuiziwia Vitalo kupenya.

Kocha mkuu wa Musongati amefunguka kuhusu mechi dhidi Vitalo na kusema kuwa amependezwa na matokeo,
"Ninaimani kila mtu amependezwa na matokeo ya leo(0-0), hakuna aliye chukiya kwa matokeo ya leo unajua kupata pointi tatu ao moja  Bujumbura ni vigumu,  mechi ya saa nane ni nzuri sana upande wangu na leo jua imekua kali"

Kuhusu kadi nyekundu ya mchezaji Sudi, kocha Vivier amesema kuwa refa amekosea na hakuwa makini pengine homa ya mechi imekuwa ngumu kwake  na kushindwa kuhamua ipasavyo,

"Kwakweli kadi nyekundu imetusumbua na unafahamu Sudi ni mchezaji mzuri kati ya wacheza wazuri wa timu yangu, na mechi kama hii ukiwa na upungufu wa mchezaji umoja inasumbua kiasi kikubwa, kwa upande wangu kadi nyekundu sio ya Sudi ni mchezaji mwingine aliye fanya kosa ila refa amemuadhibu Sudi nafasi ya mwingine, refa ameamua ivo basi tumekubali matokeo ya refa."

Wiki ya 12 ya Primus League timu ya Musongati inapangwa kuchuana na Atletico Olympic ikiwa kileleni kwenye msimomo wa Ligi, Kocha Vivier Bahati ameimbia Mishe Mishe nakusema;

 " mechi ya Atletico itakuwa Jumapili kama hawatabadili ratiba na itakuwa nyumbani Gitega, tunaiandaa vizuri na nafasi ya Sudi kuna wachezaji wengine wataziba pengo na ninaimani tutafanya vizuri pia mashabiki wetu waje kwa wingi kwa kuisapoti timu yao siku hiyo".
Powered by Blogger.