Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anaweza kuangukiwa na rungu la FA kwa kufungiwa mechi mbili

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anaweza kuangukiwa na rungu la FA kwa kufungiwa mechi mbili kutokana na utovu wa nidhamu kwenye benchi la ufundi wakati timu yake ilipokuwa ikicheza na West Ham United Jumapili hii kwenye uwanja wa Old Trafford na kutoka sare ya kufungana goli 1-1.
39fe762800000578-0-image-a-125_1478110181321
Kocha huyo alijikuta akitolewa kwenye benchi la ufundi na kupandishwa jukwaani na mwamuzi, Jonathan Moss kutokana na kitendo chake cha kupiga chupa ya maji kwa hasira baada ya Paul Pogba kuonyeshwa kadi ya njano ambayo itamfanya mchezaji huyo kuukosa mchezo wa kombe la EFL dhidi ya West Ham United Jumatano hii.
Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa Mourinho kuondolewa kwenye benchi la ufundi pamoja na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa.
Powered by Blogger.