Kocha mkuu wa timu ya taifa Burundi Olivier Niyongeko azungumzia sababu ya timu ya taifa kuonesha kiwango kibovu dhidi ya Aigle Noire

Jumapili kwenye uwanja mkuu wa MwanaFalme Louis Rwagasore timu ya taifa Intamba Murugamba  imekuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya klabu Aigle Noire kutoka Mkoani Makamba na timu zote mbili zimeridhika kwenda  sare ya bila bila (0-0).
Baada ya mechi Kocha Olivier Niyungeko amejaribu kujibu swali  kadhaa ya waandishi wa habari huku mashabiki wa timu ya taifa wameondoka kutoridhishwa na kiwango cha  wachezaji walio itwa kwa kuandaa michuano ya CECAFA.

Aidha, kocha amesema kuwa katika wiki  moja ni vigumu kuandaa timu na isitoshi wachezaji wote ni wapya huku akidai kuwa Burundi kuna tatizo kubwa ya kukosa washambuliaji na ndio sababu ya Burundi kutokufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa.

Kocha Olivier Niyungeko ameongeza na kusema kuwa kwasasa anakwenda kuundaa timu na kuwafundisha hasa washambuliaji mbinu ya kupenya walinzi wa timu pinzani.

Alipo ulizwa swala ya kuita wachezaji  wa nyumbani kuliko wachezaji wanao cheza mpira wakulipwa nje ya nchi, amefunguka na kusema kuwa
Tumeamua kuita wachezaji wa nyumbani kuliko wa nje kwasababu tumekwisha wazowea tangu 2004 tumewaona na matokeo nafikiri mumeyapata. Basi ni mda wa kuunda timu mpya pengine itakuja kufanya vizur siku za mbele, musisahau kuna michuano ya kuwania kufuzu Chan ila ni mda muafaka wakuwahanda hawa. Nimechukulia wachezaji walio itwa na Omar Ntakagero na wengine nimeongezea nafikiri ni vijana wazuri kinacho salia nikuwaanda vizuri ili tuone kama wanaweza kuwakilisha nchi vilivyo.

Kocha Olivier Niyungeko amemalizia na kutowa wito kwa watangazaji wote na kusema kuwa endapo  watangazaji wa michezo wameona wachezaji wazuri hawakuitwa basi anawaomba wawalete hawo wachezaji kwenye mazoezi ili  aone kama wanaweza kusaidia nchi yao kuliko kwenda kwenye vipindi kusema mengi  huku akisisitiza nakusema  ni mda wakujenda sio mda wakulahumiana.
Powered by Blogger.