TANGAZO
_92389799_img-20161111-wa0000-1
Yanga walipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.
Ruvu Shooting ndio walianza kuzifumani nyavu za Yanga kwa bao la Abdulrahman Mussa kwenye dakika ya saba ya mchezo.
Winga wa Yanga Simon Msuva akaisawazishia timu yake bao hilo kwenye dakika ya 32, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 56 kipindi cha pili.
Yanga wanasalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 33, huku wapinzani wao Simba wakiwa kileleni kwa alama 35.
Ligi kuu inasimama kwa muda na mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Desemba, mwaka huu.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top