Msanii wa nyimbo za injili Kezzo Ildephonse  kutoka Burundi anaetamba na nyimbo ya "Nakuja Kwako", anatarajia kuachia kolabo amefanya na mwana hip hop Tresor Shuja muimba nyimbo za injili kutoka pia Burundi, nyimbo itakuja kwajina la "OYA" chini ya mikono ya Producer Pichen.

Akizungumza na Afrianmishe, muimba nyimbo za injili Kezzo amesema kuwa amemfahamu Tresor Shuja tangia muda mrefu na kuongeza kuwa Tresor Shuja ni mwana hip hop mkubwa mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, hivo amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kupata maneno ya kuwaelimisha katika maisha wanao amini kuwa Mungu anaweza.

Aidha, Kezzo amesema kuwa mwaka wa 2017 utakuwa ni  mwaka wakufanya mabadiliko makubwa katika muziki wake wa Gospel  kwa kuachia kazi nzuri ambazo zitawakonga  nyoyo  mashabiki wake.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top