Kenya yakanusha ripoti ya UN kuhusu biashara haramu Somalia

Serikali ya Kenya imekanusha madai ya Umoja Wa Mataifa kuhusu ripoti iliyochapisha kuwa Kenya inatumia jeshi lake kuunganisha biashara haramu ya makaa nchini Somalia .

Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amekosoa ripoti hiyo na kusema kuwa utafiti uliofanywa na UN si wa kweli.

Wanajeshi wa Kenya wanaopelekwa Somalia kushiriki katika operesheni ya umoja wa Afrika (AMISOM) kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab nchini humo .

Siku ya Jumapili kitengo cha UN cha uchambuzi wa matukio maalum kilichapisha ripoti iliyodai kuwa wanajeshi wa Kenya nchini Somalia wanaruhusu uuzaji wa nje wa makaa kinyume na sheria kutoka bandari ya Kismayu .

Aidha ripoti hiyo ilibainisha kuwa wanajeshi wa Kenya pia wanapokea dola 2 kutoka kila mfuko wa makaa na kuendeleza biashara ya sekta ya makaa isiyo chini ya ukaguzi wa idara yoyote ya serikali.

Vile vile ripoti hiyo pia imekadiria pia takriban mifuko milioni 6 husafarishwa kila mwaka kutoka Kismayu hadi Buur Gaabo ambayo ni kambi nyingine ya jeshi la Kenya nchini Somalia .

Mnamo mwaka 2012 mauzo ya nje ya makaa yalipigwa marufuku na baraza la usalama la UN katika jitihada za kumaliza njia zote zinazotumiwa na Al Shabab kupata fedha .
Powered by Blogger.