Kampuni ya mawasiliano ya Google kufungua makao makuu nchini Uingereza

Ofisi ya kampuni ya Google iliyoko London Uingereza

Kampuni ya mawasiliano ya Google inafungua makao yake makuu jijini London nchini Uingereza hatua ambayo itatengeneza ajira 3000 mpaka ifikapo mwaka 2020.
Ujio wa habari hiyo ni mafanikio makubwa kwa sekta ya teknoloJia nchini Uingereza.

Mkurugenzi mtendaji wa Google, Sundar Pichai, ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza  BBC kuwa Uingereza bado ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.

Amesema kufungua kwa mipaka na uingiaji huru kwa wahamiaji wenye ujuzi ni suala muhimu kwa mafanikio ya tekinolojia nchini Uingereza.
Powered by Blogger.