JUDIE CAELLE awataka watangazaji wenzake kuwa na tamaduni wa kuchangamkia vitu vya kwao.

Mtangazaji wa kipindi cha muziki ''Ahabona moment'' kwenye Radio Colombe nchini Burundi GAHIMBARE Judie Caelle,awataka watangazaji wenzake kua na utamaduni wa kuchangamkia vitu vya kwao badala ya kukimbilia nje ya nchi.
Asilimia flani ya muziki wa Burundi unarudishwa nyuma na watangazaji ambao kazi zao nikuzicheza na kutangaza kazi za wasani wa nje ya Burundi na kuwasahau wasani wa nyumbani.Watangazaji wanauwezo mkubwa wakuwashawishi raia kupenda muziki.

'' Watu wameshindwa kuamka na kuona cha kwetu na kukichangamkia sijui kwanini kumekua na ugumu labda wanataka umaarufu zaidi nje ya nchi kuliko nyumbani.Wasani nchini Burundi wanaweza na wanajua sanaa ila sioni kinachowafanya wakimbilie nje,kazi zao ni kuwaboda na kuwakatisha tamaa wasani chipukizi kuliko kuwaonyesha ni njia gani yakupitia.


Watangazaji wengi wakisikia msani wa nje anatarajia kuingia Burundi basi iyo ndio itakua headlines yao ya mwezi mzima kwenye Radio,TV na mitandao ya kijami na wanatakua wakwanza kwenda kumpokea kwashangwe na vigeregere uwanja wa ndege na full interview,ila wanyumbani akiingia kutoka ugenini unazani hakuna chochote kimeingia.Watangazaji tuwe na uzalendo''.Alisema Judie Caelle.


Powered by Blogger.