responsive ads

Jeshi la Polisi Mkoani Singida linawashikilia watu wawili kwa kuwatishia kuwaua kwa risasi waandishi wa habari mkoani humo

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mayala Towo.

Jeshi la Polisi Mkoani Singida linawashikilia watu wawili kwa kuwatishia kuwaua kwa risasi waandishi wa habari mkoani humo ambao walitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu tukio la wizi na udhalilishaji lililofanywa na watuhumiwa hao.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mayala Towu amewataja watuhumiwa hao ambao ni Hussein na Hassan ambao wanadaiwa kuvamia katika ofisi ya chama cha waandishi wa mkoa wa Singida na kutoa maneno ya vitisho kwa waandishi hao.

Watu hao wanadaiwa kuwa waliwaambia waandishi hao kama wataendelea kutoa taarifa zao basi watawadhuru wao na familia zao ndipo waandishi hao walipochukua hatua ya kuripoti tukio hilo polisi na hatimaye watuhumiwa hao kushikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda Mayala amesema kuwa baada ya kuwashikilia watu hao walifanya msako katika makazi yao na kuwakuta na bunduki mbili aina ya rifle hivyo waliwashikilia kwa muda na kuwafungulia kesi ili kujibu tuhuma hizo.
middle 300x250
Powered by Blogger.