Hakizimana Ramadhan aomba wadau kusapoti vijana wa cadet

Mwenyekiti wa soka la vijana wasio zidi umri wa miaka 17 Cadet Buyenzi, Hakizimana Ramadhani akijulikana kwajina la Dokta Ramaya, aomba wadau wa soka kusapoti vijana kwa kuendeleza vipaji  vya vijana ili wazidi kuendelea mbele katika maisha yao ya soka.

Mwenyekiti  huyo ameiambia africanmishe kuwa wamejitaidi kujiunga na baadhi ya kampuni ila hazikuwapa sapoti yoyote, kwa hiyo anaomba warundi wote kwa jumla wawape sapoti kubwa ili wafanikishe malengo ya vijana hawo wanao jituma katika soka.

Hakizimana Ramadhani ( Dokta Ramaya) aliwasihi  na kuwaomba wale wachezaji walio pitiya katika shirikisho la Cadet Buyenzi na leo wanacheza mpira wakulipwa nje, wajitokeze kwa kuwasapoti vijana huku akisisitiza kuwa vijana hawa ndio timu ya taifa ya kesho basi ni mda wa kuwa sapoti ili tupate timu ya taifa yenye wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
Powered by Blogger.