responsive ads

Exclusives:DJ PRO anatarajia kufanya Bonge la tamasha ''VIP ALL WHITE PARTY'' nchini Burundi December.

Baada ya kukosa tuzo za AEA-USA Awards mwaka huu kwenye kipengele cha Best New Talent na kunyakuliwa na mwadada LIPSIA  kutoka nchini Angola,DJ PRO hakukata tamaa na anatarajia kufanya bonge la tamasha litwalo ''V.I.P ALL WHITE PARTY'' nchini Burundi ambalo litafanyika tarehe 17 December 2016.

Kwenye tamasha hilo Dj Pro amewaalika mastaa wengine ambao wanafanya vizuri kwasasa kwenye game la muziki nchini Burundi,kama : Black G,Emery Sun,Kebby Boy na Mr Champagne.
Tamasha la V.I.P ALL WHITE PARTY litafanyikia kwenye ukumbi wa HAVANA NIGHT CLUB na kingilio itakua ni 25000 Pesa ya Burundi unapewa chakula na kinywaji na 50000 VIP Place unapewa chakula kinywaji na kujipigisha picha na mastaa wa kubwa nchini humo.
Dj Pro kwasasa anazichapa kazi zake za muziki nchini South Africa mjiini Cape-Town.
Hit maker huu wa kibao ''Maisha na Muziki'' amewalika mashabiki zake na wapenzi wa muziki Afrika mashariki kujitokeza kwawingi kushirikiana nae, na patakuwepo surprise kibao na itakua ni fursa yake kuwaonesha Manager zake wanaomsaidiza kazi zake za muziki.

Tovuti yako ya africanmishe.com itaendelea kukujuza mara kwa mara maandalizi ya tamasha hilo liloandaliwa na DJ PRO NEGGER.

Itazame hapa video yake ya Maisha na Muziki ambayo inazidi kufanya vizuri barani Afrika.
Bonyeza kitufe cha Play hapo chini.


middle 300x250
Powered by Blogger.