responsive ads

Diamond adai Ommy Dimpoz amemtafuta mara kibao wayamalize akamtosa

Diamond amefunguka kuhusu jitihada zilizowahi kufanywa ili kumaliza bifu lake na Ommy Dimpoz.
15099356_1262691977129629_174413472224772096_n
Ni muda mrefu wawili hao wamekuwa hawaelewani japo hakuna aliyewahi kuweka wazi chanzo cha ugomvi huo. Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond amethibitisha kuwa aliwahi kutafutwa na Dimpoz pamoja na kuwatuma watu ili wayamalize.
“Kashatuma watu wengi sana, kashamtuma Sallam, alishanipigia mpaka na simu nikashindwa kupokea nitaongea naye nini,” alisema.
“Mipaka ilivuka halafu mimi ni muislam. Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu,” aliongeza.
Hata hivyo wakati Diamond akihojiwa, Ommy Dimpoz alitweet kukanusha alichokisema.
“Aisee kumbe @Sallam_SK kila siku unavyonibembeleza tuyamalize na Mwana kumbe nakutuma kweli nyie profeshenooo ,” ametweet Ommy.
“Wazee @BDozen @CloudsMediaLive Naombeni Kipindi Kesho ,” ameongeza.
Wakati huo huo Sallam amemjibu Ommy: Sijakuomba mie! Kumbuka aliyekwambia nani Na mie nilijibu nini? Hata wakati ulipokuja kuomba yaishe na mie kumbuka nani alikuleta!
Bifu ya Ommy na Diamond imeongezeka zaidi kuanzia jana baada ya kutoka kwa wimbo wa Rich Mavoko ‘Kokoro.’ Wawili hao wametupiana vijembe kwenye Instagram.
middle 300x250
Powered by Blogger.