responsive ads

Chadema kuja na oparesheni ya ‘Kata Funua’

Baada ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia Chadema kuanzisha umoja wa kupinga udikteta Tanzania (UKUTA), Chadema imekuja na oparesheni nyingine inayokwenda na jina linaloitwa ‘Kata Funua’
mbowe
Jina hilo limetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kanda wilayani hiyo huku akidai lengo la oparesheni hiyo ni kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo baadaye.
Kwa upande wake, Mjumbe wa kamati kuu Chadema, Edward Lowassa aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa na umoja ili kufanikisha azma hiyo.
“Nawaomba ndugu zangu tuungane chini ya mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na viongozi wengine tusimame imara tukiongoze chama chetu kwa umoja na mshikamano,” alisema.
middle 300x250
Powered by Blogger.