Amical : Ivory Coast itakabiliwa na Ufaransa katika mechi ya Kirafiki Jumanne hii

Timu ya taifa Ivory Coast itakabiliana na timu ya taifa Ufaransa katika mazingira ya mechi ya kirafiki Jumanne Novemba  15 kwenye uwanja wa Felix Bollaert, Lens.

Hii itakuwa mara ya pili katika historia ya timu hizi mbili kukutana baada ya Ivory Coast kupoteza kwa bao 3 bila dhidi ya Ufaransa tarehe 17 Agosti 2015 kwenye uwanja wa Mosson ya  Montpellier.

Ivory Coast leo Jumamosi itapambana na Morocco katika wiki ya pili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2018 kabla ya kucheza na Ufaransa.

Tuwakumbushe kuwa Ivory Coast itakuwa na pengo kubwa ya kuwakosa wachezaji wake kwenye mapambano haya, kama Gervinho, Eric Bailly, pia nahodha, Jean Michel Seri.

Powered by Blogger.