responsive ads

mesothelioma settlements amounts

Watu zaidi ya 21 wamekufa kwa ugonjwa wa ajabu.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo
 Na. Vero Ignatus Arusha
Wakati watu zaidi ya 21 wamekufa katika kata ya Pinyinyi wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha kwa ugonjwa wa ajabu wa kutapika damu,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Frida Mtiki hana taarifa juu ya kuwepo kwa ugonjwa huo.

Hayo yalisemwa na Mtendaji wa kata hiyo,James Mushi wakati akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alipokwenda kutembelea kata hiyo kujionea shughuli za maendeleo ikiwa ni ziara ya siku tano katika wilaya hiyo.

Baada ya Mushi kueleza katika risala yake juu ya kuwepo kwa ugonjwa huo kwa zaidi ya miaka minne na watu 21 kupoteza maisha ndipo Mkuu wa Mkoa alipomsimamisha Mganga Mkuu wa Mkoa ili kupata maelezo ya kwa nini Mkoa haujachukuwa hatua.

Mganga huyo alisimama na kuueleza umma wa wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa hadhara kuwa hana taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo na wala Mkoa haina taarifa juu ya kuwepo kwa ugonjwa huo.

Majibu hayo yalimchanganya na kumkasirisha Mkuu wa Mkoa na kuamua kumsimamisha Mganga wa Wilaya ya Ngorongoro(DMO),Omari Sukari kutoa majibu kama na na yeye hana taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo.

Sukari alikiri kuwepo kwa ugonjwa huo na alikiri kweli umeua watu 21 na amefanya jitihada na ziada kwa kupeleka sambo Wizara ya Afya kwa wataalamu kwani hata yeye ameshindwa kujua nini chanzo cha ugonjwa huo na kina sababishwa na kitu gani.

Mganga huyo wa wilaya alisema vipimo vya awali vilionyesha kuwa ugonjwa huo husababishwa na ugonjwa wa kichocho lakini bado wamejiuliza zaidi kwa kupeleka samba nyingine ya matapishi kwa wataalamu wa magonjwa ya binadamu kujua zaidi ukweli wa ugonjwa huo na majibu hayajarudi.

Baada ya majibu hayo,Mkuu wa Mkoa alieleza waziwazi kusikitishwa na kushangazwa majibu ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kusema kuwa haingii akilini ugonjwa ulioua watu 21 na uko zaidi ya miaka minne katika kata ya Pinyinyi lakini hana taarifa wakati Mganga wa Wilaya anayo taarifa.

Gambo alisema kuwa hiyo inaonyesha wazi kuwa baadhi ya watumishi wa serikali Mkoani Arusha wanafanya kazi kwa mazoea na kushindwa kujua ama kupata taarifa za kila siku katika wilaya.

Alisema hilo hatalivumilia hata kidogo na kuwataka wakuu wa idara wa mikoani kuwajibika kwa kupata taarifa za kila siku katika wilaya zote za mkoa wa Arusha ili majibu ya kila kitu yaweze kupatikana na kupatiwa ufumbuzi wa kutosha.
­­’’Hii ni aibu ugonjwa upo kwa miaka minne na tayari umeua watu 21 lakini RMO hana taarifa lakini DMO anayo taarifa na amefanya kazi ya ziada kutafuta chanzo cha ugonjwa huu’’ alisema

’’Kama nisingekuja hapa ina maana huu ugonjwa usingejulikana wala kupata majibu ya kutosha na watu wangeendelea kufa sasa nataka RMO kuhakikisha ugonjwa huo unakwisha na dawa inapatikana’’ alisema Gambo

Katika risala hiyo wananchi wamempongeza mkuu huyo wa Mkoa wa kufika katika kata hiyo kwani mara ya mwisho Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembelea kata hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa, Mohamed Babu mwaka 2006
middle 300x250
Powered by Blogger.