Warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali watakaoshiriki miss Tanzania wawasili Arusha

 Warembo 30  kutoka mikoa mbalimbali  hapa nchi ni wanashiriki shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) wameingia Rasmi mkoani Arusha na kutembelea ofisi za gazeti la The Guardian na Nipashe  ikiwa ni moja ya kazi ambazo watazifanya wakiwa mkoani hapa.

Akizumza na waandishi wa habari  Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapa leo na wanakaa kwa muda wa siku tatu ,na katika siku hizo wanampango wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Aidha alisema kuwa pia ndani ya siku hizo tatu kutakuwa nashindano la Top model ambalo litafanyika Jumamosi October 15 katika ukumbi wa Triple A ulipo ndani ya jiji la Arusha 
"tunafanya shindano hilo katika ukumbi wa triple A natunarajia wananchi wengi wa Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo ni shilingi 10000 tu hivyo napenda kutumia mda huu kuwaalika wananchi wa Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa Top Model"alisema Makoye
Alisema kuwa  mbali na hapa warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma,Singinda ,Dar  es Salaam  hapa Arusha na hatimaye wanatarajia kuondoka na kwenda mwanza ambapo ndipo shindano hili linafayanyika kwa mwaka huu .
Alisema kuwa shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika october 29 katika ukumbi wa Rock City Mall  ambapo alibainisha adi sasa warembo wote 30 wapo vizuri na wanasubiria siku yenye ifike na maandalizi yashindano yamekamilika
Powered by Blogger.