Wanatunyanyasa sana hawo wasani wakubwa, Prince-B Expert

Msanii chipukizi wa kizazi kipya wa Burundi Flava, Prince-B Expert ameonesha maskitiko yake kwa niaba ya wasani wote chipukizi kuwa wanazidi kunyanyaswa na kushinda kufikia malengo wakati wanavipaji.

Akiwa studio akirikodi nyimbo yake mpya, ameongea na muandishi wa Mishe Mishe, Prince B amesema "yaani nashindwa kuwaelewa wasani wakubwa ambao  ni ma braza wetu  kwenye muziki na tayari wamejijengea sifa nyingi nchini wanazidi  kutunyima nafasi  sisi wasani chipukizi kama show wakati hawana nyimbo mpya pia wanatunyima collabo".

Prince B amefunguka kwanini ma staa ambao ni maarufu wanawanyanyasa  na kuwaziwia wasije kuwa juu yawo, upande wake anafikiri  kuwa wanaofia wasije kuwazimisha kwenye ulimwengu wa muziki.

"pengine wanaimani mbovu, wanafikiri tutakuja kuwazimisha huku wanasahau kuwa kila kitu na mda wake, bila hivo hata collabo wanatunyima tofauti na nch zingine. Sisi tunahinuliwa na wao kitu moja watambuwe siwezi wataja majina ila wajuwe kama umefanikisha kujenga jina basi nawe pandisha mwingine  ili sote tuitangaze nchi yetu", amesisitiza Prince B
Powered by Blogger.