Walimu wanaoiba madawati kukamatwa

Tokeo la picha la madawati
Wakati mkoa wa Manyara ukiwa na ziada ya madawati zaidi ya 3,000, mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera amewataka wadau wa elimu kuwafichua  na kuwakamata  walimu na viongozi wa serikali wanaoiba madawati kutoka katika shule za serikali na kisha kuyauza kinyemelea kwa shule binafsi ambazo zinakabiliwa na uhaba wa madawati.
Agizo hilo amelitoa wakati akikabidhi madawati 300 kwa madiwani wa kata tatu za Mwada, Nkaiti na Magara yaliyotolewa na jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori yenye vijiji 10 katika tarafa ya Burunge wilayani Babati, licha ya kusisitiza uhifadhi wa wanyamapori na mazingira, lakini amesema ofisi yake imepokea uuzaji wa madawati huo wa madawati kwa shule zilizojitosheleza.
 
Awali kabla ya kukabidhiwa kwa madawati hayo kwa serikali, katibu wa jumuiya hiyo Bw Olais Ole Koini amesema jumuiya hiyo ya juhibu imelazimika kutengeneza madawati hayo kutokana na mapato ya uwindaji wa kitalii na upigaji wa picha unaofikia zaidi ya shilingi bil 3 kwa mwaka lakini pia uhifadhi huo ukipigwa vita na baadhi ya wanasiasa.
Powered by Blogger.