WADAU WA MUZIKI MORO WAPONDA TUZO ZA ULUGURU ENTERTAINMENT AWARDS

Wadau wa muziki ndani ya mkoa wa Morogoro wameponda tuzo za Uluguru Entertainment Awards zilizoanzishwa kwa lengo kukuza vipaji vya wasanii mkoani humo zikidaiwa kutokuwa na maandalizi ya kutosha.
Kupitia Comment kwenye ukurasa wa facebook wa tuzo hizo mmoja wa wadau Ibrahim Rashid Aman amehoji "Vigezo gani mnatumia kuwaweka wanaogombania?Vipaji mnavikuza kwa staili ipi?izi tuzo jni kwa ajili ya wasanii wa morogoro au kwa ajili ya wasanii wa Tanzania? kama ni za morogoro mbona kuna wasanii wengi na atuwaoni kwenye izo tuzo zenu za kukuza vipaji?ofisi yenu ipo wapi apa Morogoro nahitaji kuja ofisini kufahamu zaidi izi tuzo zenu?.
                                                       Rajram Kipila na Mash J
Pia mmoja ya Rappers wa mkoani humo Rajram Kipila nae akadai kutoridhiswa na tuzo hizo akidai wapo artsit wengi majina yao yamejirudia na kuhoji sababu ya kuwemo kwa majina ya Man Fongo na Criss Wamarya kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka. 
Tayari tuzo hizo zimeanza kupigiwa kura zikiwa na vipengele 21 na jinsi ya kupiga kura ni kuandika jina la mshiriki kwenye account ya facebook ya  Uluguru Entertainment Awards.
Powered by Blogger.