Video: Tale atoboa siri ya usambazaji wa nyimbo za WCB, hawaanzi na redio, blogs wala runinga

Babu TALE


Moja kati ya sehemu ambayo muheshimiwa alipekekwa ni sehemu ambayo
huwa mikutano kuhusu usambazaji wa kazi za wasanii wa WCB hufanyika.Akiongea katika utambulisho huo, Babu Tale alisema wao katika
usambazaji wa kazi za wasanii wao huanza kwa watu wa chini ambao
wanapatikana mtaani.


“Hii ni ofisi ya watu wa creative,” alisema Tale katika ubambulisho
huo. “Wakati wa kunatoa nyimbo mpya lazima tunakaa na kuwaza tunafanya
nini na tutatoa kwa style gani ili tuanze kuukamata mtaa tunafanyaje
kuhusu mtaa. Kwa hiyo tunapotoa nyimbo tunahakikisha kila mtu mtaani
anayo halafu ndio tunaiachia redioni. Kwahiyo ikienda redioni watu wa
mtaa watakuwa wanaisukuma ile ya redio,”


Pia Diamond alisema wanaitegemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa katika kusambaza nyimbo zake kwa uharaka zaidi.


Kwa upande wa Waziri January Makamba alimmwagia sifa Diamond pamoja na team yake kwa kufanya kazi nzuri.

Powered by Blogger.