VIDEO : INTER STAR VS MESSAGER BUJUMBURA ( 0-1), MAAMZI YA REFA NA REFA MUSAIDIZI

 Mechi kati ya Inter Star dhidi ya Messagé Bujumbura imezuwa utata mpaka homa ya asira imewashika mashabiki wa Inter Star na wachezaji pia kwa kile ambacho Inter Star imedai kuwa refa wa mechi hiyo amechukua maamzi mabovu ya kumaliza mechi mapema huku dakika nyingi zimepotea kwenye mechi hiyo ata hivyo hazikuongezwa.
Kama mtakavyo shuhudia kwenye video hii, mchezaji wa Message Buja ameumia na ameitaji kutibiwa  nje ya uwanja ila wachezaji wenza na refa wamekataa atoke nje ili atibia wakati Inter Star ipo kwenye arakati ya kutafuta goli ya kusawazisha.
Baada ya vurugu takriban dakika 3, refa musaidizi ameingia uwanjani na kumuambia refa mkuu amalize mechi mapema, maamzi ayo ndio imezidi kuwapa homa ya asira wachezaji pia mashabiki wa Timu Inter Star na kudai kuwa refa mkuu na msaidizi wake  wamechukua maamzi mabovu.

Tuwakumbushe kuwa itakua mechi ya tano Message Bujumbura ikiitambia Inter Star huku Inter Star inazidi kutafuta mfumo mwingine kwa kuidhibiti timu hii.
Powered by Blogger.